#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amehitimisha mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 15 katika eneo la Kariakoo, ukihusisha familia ya marehemu Abdallah Sultani Mtambo na Bw. Salim Selemani Salim.
RC Chalamila amemkabidhi rasmi Bw. Salim nyumba namba 12, kiwanja namba 15, baada ya kujiridhisha kuwa aliinunua kihalali kupitia mnada wa mahakama mwaka 2011 kwa gharama ya shilingi milioni 250.
Uamuzi huo umetokana na taarifa ya kamati maalumu iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa, ikiongozwa na Mwanasheria Fabiola Mwingira, ambayo ilibaini kuwa taratibu zote za kisheria zilifuatwa baada ya warithi kutoelewana.
Imeelezwa kuwa baadhi ya warithi walishapokea sehemu ya fedha za mauzo hayo, huku kiasi cha shilingi milioni 64.5 kilichokuwa kimegomewa na baadhi ya warithi kimeelekezwa kurejeshwa mahakamani ili kikabidhiwe kwa wahusika kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, amemshukuru RC Chalamila kwa kumaliza mgogoro huo uliokuwa kero ya muda mrefu jimboni humo.
Mpogolo ameahidi kuwa kamati ya usalama ya wilaya itahakikisha amani inadumishwa katika eneo hilo ili mmiliki halali aweze kuendelea na shughuli zake bila bughudha yoyote, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu maamuzi ya mahakama.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania