#HABARI: Nchi ya Nigeria inasema takriban wanajeshi mia moja wa Marekani wamewasili kusaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wake.

Nigeria iliomba usaidizi wa mafunzo, kiufundi na ushirikiano wa kijasusi baada ya Rais Trump kuishutumu kwa kushindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya mashambulizi kijihadi.

Msemaji wa ulinzi wa Nigeria amesema takriban wanajeshi 100 wa Marekani wamewasili nchini Nigeria huku Marekani ikiimarisha operesheni ya kuwalenga waasi wa Kiislamu.

Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumu Nigeria kwa kushindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Hata hivyo, Nigeria imekanusha kubagua dini yoyote ikisema vikosi vyake vya usalama vinalenga makundi yenye silaha ambayo yanashambulia pande zote mbili Wakristo na Waislamu.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *