#HABARI: Viongozi na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamefanya ziara ya kikazi katika Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), ambapo wamepongeza matumizi sahihi ya kodi za Watanzania.

Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano wa TRA, Bw. Richard Kayombo, ameeleza kuwa mradi huo ni ushahidi tosha wa namna fedha za walipakodi zinavyobadilisha maisha ya wananchi kwa kuleta maendeleo makubwa yanayoonekana na kugusa jamii moja kwa moja.

Ziara hiyo iliyoshirikisha maafisa mawasiliano kutoka vituo vyote nchini, ililenga kuwajengea uelewa wa jinsi miradi ya kimkakati inavyotekelezwa kwa kodi za ndani.

Maafisa hao wameahidi kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari, wakisisitiza kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya nishati utasaidia kuondoa changamoto za umeme, kukuza biashara, na kupanua wigo wa mapato ya Serikali kupitia uwekezaji na uzalishaji viwandani.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Kituo hicho, Mha. Elinainyi Kalalu, amewahakikishia viongozi hao kuwa mradi utaendelea kuzalisha umeme kwa weledi ili kufikia lengo la megawati 2,115.

Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya TRA na sekta ya nishati ni muhimu, kwani kodi ndizo zinazowezesha ujenzi wa miundombinu hiyo ya kisasa inayohakikisha huduma bora ya umeme kwa Watanzania na kuleta ustawi wa taifa kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *