#HABARI: Watu wanne wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Itekesha Kata ya Kilesha wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji ya Mto Kagera, wakati wakiwa ndani ya nyumba yao kufuatia mto huo kufurika na kuacha njia yake ya asili, kisha kuelekea kwenye makazi ya wananchi.
Wakizungumza katika nyakati tofauti wakazi wa kijiji hicho, wamesema chanzo ni mvua kubwa kunyesha na kusabaisha mto Kagera kusomba makazi ya familia hiyo na kusababisha vifo vyao hapo papo.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa SACP Shadrack Masija, amethibitha kutokea kwa kutukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wanaoishi kando ya mito kuchukua tahadhari.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.