#HABARI: Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amewataka wathibiti ubora wa shule kutoka halmashauri 184 nchini kushirikiana kwa karibu na walimu katika kutekeleza mkakati wa kitaifa wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu).

Akizungumza mjini Bagamoyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa maafisa hao, Prof. Mkenda amesisitiza kuwa ushirikiano huo ni nguzo muhimu katika kuleta mageuzi makubwa ya elimu yenye tija na ubunifu kama ambavyo Watanzania wanatarajia kwa maendeleo ya taifa.

Aidha, Prof. Mkenda amebainisha mpango wa Serikali wa kuongeza madarasa ya sekondari ndani ya shule za msingi ili kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari.

Maafisa uthibiti ubora wa shule wamepongeza hatua hiyo na kuahidi kusimamia viwango vya elimu kwa umakini zaidi, huku wakieleza kuwa mafunzo hayo yatawaongezea mbinu mpya za kuhakikisha ubora wa elimu unaimarika kuanzia ngazi za halmashauri zote nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *