
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary
Clinton, ameishutumu
serikali ya Rais Donald Trump kwa “kuficha ukweli” kuhusu jinsi
ilivyoshughulikia faili zinazohusiana na marehemu Jeffrey Epstein, mhalifu wa
ngono.
“Zitoe
faili hizo. Wanapeleka jambo hili polepole,” waziri huyo wa zamani wa
mambo ya nje wa Marekani aliambia BBC huko Berlin, ambapo alihudhuria Kongamano
la Dunia la kila mwaka.
Ikulu ya
White House ilisisitiza kwamba kwa kutoa faili hizo walikuwa wamewafanya jambo
kubwa “zaidi kwa waathiriwa kuliko kile ambacho Democrats imewahi kufanya”.
Alipoulizwa ikiwa
Andrew Mountbatten-Windsor anapaswa kuwasilisha kesi mbele ya kamati ya bunge,
Hillary Clinton alisema: “Nadhani kila mtu anapaswa kutoa ushahidi kwa
anayeombwa kutoa ushahidi.”
Kuonekana
kwenye faili si dalili ya kutenda makosa. Andrew amekuwa akikanusha kufanya
makosa yoyote.
Mamilioni ya
faili mpya zinazohusiana na Epstein ziliwekwa hadharani na idara ya sheria ya
Marekani mapema mwezi huu baada ya Bunge kupitisha sheria inayoitaka Idara hiyo
kutoa taarifa zinazohusiana na uchunguzi wa Epstein.
Bi Clinton na mumewe, rais wa zamani Bill Clinton,
wamekubali kutoa ushahidi katika uchunguzi wa bunge kuhusu mhalifu wa kingono
marehemu Epstein.
Bill Clinton
atafika tarehe 27 Februari, na Hillary Clinton atafika siku iliyotangulia.
Rais Trump amekanusha mara kwa mara kufanya makosa na
kusema aliachana na Epstein miaka mingi iliyopita.
Bill Clinton
– ambaye ametajwa mara kadhaa katika faili za Epstein – alikuwa akimfahamu
Epstein, ambaye alifariki gerezani mwaka wa 2019, lakini anasema alikata
mawasiliano miongo miwili iliyopita.
Soma zaidi: