Jumla ya Shilingi Bilioni 2 zimetolewa kwa wajasiriamali wa Jimbo la Mtumba, mkoani Dodoma, kwa lengo la kuwawezesha kupata mitaji nafuu na kujikwamua kutoka kwenye mikopo isiyo rasmi yenye riba kubwa maarufu kama “kausha damu”.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo hiyo Februari 17, 2026, Mbunge wa Mtumba na Waziri wa Madini, Antony Mavunde, amesema fedha hizo zinalenga kuongeza mtaji kwa wajasiriamali wa jimbo hilo na kukuza biashara zao katika mazingira yenye masharti nafuu.
Katika hatua nyingine ya uwezeshaji kiuchumi, CRDB Foundation kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia COSTECH, wametenga Shilingi Bilioni 4.6 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wenye biashara changa na wabunifu kupanua shughuli zao.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)