
Kamishena wa Ulaya anayehusika na Misaada ya Kibinadamu amewasili jijini Kinshasa ikiwa ni hatua ya kwanza katika ziara itakayompeleka katika nchi kadhaa katika eneo la Maziwa Makuu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwenye agenda, DRC, Burundi na Rwanda. Tangu kutekwa kwa Goma na kundi lenye silaha la AFC/M23 mwaka mmoja uliopita, wale wanaofanya kazi katika maeneo ya matukio wamekuwa wakitoa tahadhari mara kwa mara kuhusu kupunguzwa kwa ufikiaji wa misaada ya kibinadamu.
Wasiwasi hii inaungwa mkono pia na Hadja Lahbib, ambaye hivi karibuni alirejelea wito wake wa ufikiaji kamili na usio na vikwazo wa misaada ya kibinadamu. Ujumbe huu utakuwa muhimu kwa mikutano yake na mamlaka mbalimbali katika siku zijazo.
“Ninakusudia kukutana na pande zote kwenye mzozo,” Kamishna wa Ulaya aliambia shirika la habari la Ubelgiji Belga, akiongeza kuwa “lengo ni kupata ufunguzi wa njia salama ili kutoa msaada kwa mamia ya maelfu ya watu walioathiriwa na mzozo huu, ikiwa ni pamoja na katika maeneo yanayodhibitiwa na vikundi vyenye silaha.”
Baada ya Kinshasa Jumanne, Kamishna wa Ulaya atakuwa Burundi Jumatano na Alhamisi. Amepangwa kutembelea kambi ya wakimbizi ya Busuma, ambapo hali ya maisha ya wakimbizi wa Kongo, hasa kutoka Kivu Kusini, ni mbaya sana, maji na chakula ni haba sana.
Baadhi ya familia hazina hata maturubai ya makazi. Hatimaye, Kamishna wa Ulaya atahitimisha ziara yake Ijumaa kwa ziara ya Kigali, nchini Rwanda.