Watu karibu thelathini wameuawa katikati ya nchi ya Sudan, baada ya ndege isiyokuwa na rubani kushambulia soko, katika eneo ambalo wanajeshi na wanamgambo wa RSF wameendelea kupambana.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea katika ngome ya RSF katika jimbo la Kordofan, ambalo kwa miaka mitatu limeendelea kushuhudia mapigano makali.

Kwa mujibu wa mashuhuda na watetezi wa haki za binadamu, shambulio hilo la Jumatatu, lililenga soko la al-Safiya linalopatikana nje kidogo ya mji wa Sodari.

Walioauwa ni wanawake, watoto na wazee waliokuwa sokoni wakati ndege hiyo isiyokuwa na rubani, iliyoporusha mabomu, na mpaka sasa haijafahamika iwapo ni jeshi au wanamgambo wa RSF waliotekeleza shambulio hilo.

Jimbo la Kordofan, limeshuhudia ongezeko la mashambulio ya mabomu kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani kutoka pande zote, katika vita vya kudhibiti eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *