Mchungaji wa Marekani Jesse Jackson, mtetezi mwenye bidii wa haki za Wamarekani Weusi na mshirika wa karibu wa Martin Luther King Jr., amefariki akiwa na umri wa miaka 84, familia yake imetangaza katika taarifa siku ya Jumanne, Februari 17. “Kujitolea kwake bila kuteterek kwa haki, usawa, na haki za binadamu kusaidia kuunda harakati za kimataifa za uhuru na utu,” familia yake imesema, ikiongeza kwamba amefariki “kwa amani siku ya Jumanne, akiwa amezungukwa na familia yake.”

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mchungaji huyo Mweusi alifariki “kwa amani” Jumanne, Februari 17, akiwa amezungukwa na wapendwa wake baada ya vita virefu akisumbuliwa na ugonjwa wa Parkinson, familia yake imetangaza kwenye Instagram. “Akiwa kama mwanaharakati wa mabadiliko, aliwapa sauti wasio na sauti […] na kuacha alama isiyofutika katika historia,” familia yake imeongeza.

Akiwa amezaliwa nchini Marekani, wakati huo ikiwa na vitendo  vya ubaguzi wa rangi, Mchungaji Jesse Jackson alishiriki katika baadhi ya vipindi muhimu zaidi vya kupigania usawa wa rangi nchini Marekani.

Alikuwa Memphis na Martin Luther King Jr. mnamo mwaka 1968 wakati mwanaharakati huyo mtetezi wa haki za kiraia aliuawa. Alisimama huku akilia, baadae akakaa kimya, miongoni mwa umati wa watu wakisherehekea ushindi wa Barack Obama mwaka wa 2008. Alikuwa na familia ya George Floyd mwaka wa 2021, baada ya hukumu ya kihistoria kumkuta afisa wa polisi Mzungu, Derek Chauvin, na hatia ya mauaji ya mwanamume huyo Mmarekani Mweusi.

Mchungaji Jackson alipata umaarufu katika miaka ya 1960 akifanya kazi chini ya Martin Luther King Jr. kwa Mkutano wa Uongozi wa Wakristo wa Kusini, shirika lilnalopigania haki za kiraia kwa roho ya kutotumia vurugu, kabla ya kuanzisha harakati zake mwenyewe, Operesheni Push, ambayo sasa inajulikana kama Push Rainbow. Shirika hili linatetea haki za wachache, hasa haki za kupiga kura, na pia amesaidia kifedha familia nyingi za watu weusi walio katika hali ngumu na kufadhili elimu ya maelfu ya watoto.

Kampeni mbili za urais

Muda mrefu kabla ya Barack Obama, Jesse Jackson aligombea katika kura za mchujo za chama cha Democratic kwa uchaguzi wa urais wa 1984 na 1988. Alikuwa Mmarekani Mweusi wa kwanza kupata mafanikio makubwa, akipata 20% na kisha 30% ya kura. “Wapiga kura wangu ni wale waliokata tamaa, waliotengwa, walionyimwa haki, waliopuuzwa, waliodharauliwa, wanyonge,” mchungaji huyo wa Kibaptisti alitangaza katika Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa chama cha Democratic wa mwaka 1984. Ilikuwa kupitia kampeni zake mbili za urais ambapo alipata umaarufu, akipanua jukwaa la kisiasa la chama cha Democratic ili kujumuisha mapambano ya Wamarekani Weusi. Mnamo mwaka 1988, alitoa taswira ya kudumu, haswa kwa hotuba kuhusu “msingi wa pamoja,” akiwahimiza Wamarekani kuungana. “Mrengo wa kushoto, mrengo wa kulia … unahitaji mabawa mawili kuruka.” Akishambulia rekodi ya Ronald Reagan, Jesse Jackson alilaani ukosefu wa usawa wa mfumo aliouita “Robin Hood kinyume chake,” akiwapendelea matajiri zaidi na kuwaacha maskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *