NANAUKA CUP YAANZA KUWAKUTANISHA VIJANA MTWARA

Mbunge wa Mtwara Mjini ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel nanauka ameanzisha mashindano ya michezo yanayojulikana kama Joel Nanauka Cup, yakilenga kuwakutanisha vijana, kujadili changamoto zinazowakabili na kuhamasisha afya kupitia michezo.

Mashindano hayo yamekusanya timu za vijana kutoka maeneo mbalimbali jimboni humo yakitoa jukwaa la kuimarisha mshikamano wa kijamii na kukuza vipaji vya michezo.

Akizungumza kuhusu udhamini wa mashindano hayo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Huduma kwa Vijana wa Benki ya CRDB, Mshindo Magimba, amesema benki hiyo imeunga mkono mashindano hayo kama sehemu ya juhudi zake za kuwainua vijana kiuchumi na kijamii.

Licha ya kudhamini ligi na michuano mbalimbali nchini ikiwamo Kombe la Shirikisho na Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (Taifa Cup), Benki ya CRDB huandaa mashindano kwa ajili ya wafanyakazi wake yaitwayo Super Cup pamoja na mbio za hisani za CRDB Bank Marathon zinazowakusanya wakimbiaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVSports

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *