Nchini Nigeria, wanajeshi 100 wa Marekani wapo nchini humo katika ushirikiano wa operesheni za kiusalama kupambana na makundi ya kijihadi na kigaidi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya ulinzi nchini Nigeria, imesema wanajeshi hao wa Marekani wamekuja kutoa mafunzo, lakini haijatoa taarifa za kina kuhusu kuwasili kwao.

Hatua hii imekuja, baada ya serikali ya Nigeria, kuomba Marekani kusaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wake na kutoa msaada wa vifaa ili kukabiliana na magaidi.

Rais Donald Trump amekuwa akidai kuwa Wakiristo nchini Nigeria walikuwa wanalengwa na magaidi.
Rais Donald Trump amekuwa akidai kuwa Wakiristo nchini Nigeria walikuwa wanalengwa na magaidi. REUTERS – Jonathan Ernst

Ushirikiano huu pia unakuja baada ya jeshi la Marekani mwezi Desemba mwaka uliopita, kutekeleza mashambulio ya angaa katika jimbo ma Sokoto, kuwalenga wanajihadi baada ya rais Donald Trump kudai kuwa Wakiristo nchini Nigeria walikuwa wanalengwa na magaidi.

Kwa muda mrefu sasa Nigeria, imeendelea kukabiliwa na makundi ya kigaidi kama Boko Haram, Kaskazini mwa nchi hiyo na makundi mengine ya kijihgadi ambayo yameendelea kuwauwa na kuwateka raia wa kawaida na maafisa wa usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *