
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kumaliza changamoto za usafiri na usafirishaji wa mizigo katika Kisiwa cha Pemba.
Akizungumza leo, Februari 17, 2026, wakati wa ufunguzi wa Msikiti mpya wa Chachani, uliopo Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, Rais Mwinyi amesema Serikali imeandaa meli mbili za mwendo kasi na ipo katika hatua za kupata meli maalum ya mizigo kwa safari kati ya Unguja na Pemba. SOMA: Rais Mwinyi azindua Mji wa Dk. Hussein Mwinyi

Aidha, ameeleza kuwa meli ya MV Mapinduzi II itaanza kazi hivi karibuni baada ya kukamilika kwa matengenezo kadhalika na uboreshaji wa bandari za Pemba utachochea uwekezaji wa sekta binafsi katika kuongeza vyombo vya usafiri. Katika hatua nyingine,Rais Mwinyi amewahimiza waumini kutumia misikiti kujadili changamoto za kijamii na kuwataka wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula wakati wa mfungo wa Ramadhan.