
UJENZI wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 na upana wa mita 41 unaeendelea mkoani Dar es Salaam.
SOMA: Mambo yaiva ujenzi daraja Jangwani
Wizara ya Ujenzi imesema ujenzi wa daraja hilo unahusisha misingi ya daraja (piles na pile caps), nguzo kuu (piers) na maandalizi ya eneo la juu la kupitisha watumiaji (deck).

Aidha, daraja hilo litakuwa na jumla ya nguzo za msingi takribani 496 zenye urefu wa mita 35 hadi 42 chini ya ardhi kulingana na tathmini ya udongo ambapo hadi sasa nguzo 404 tayari zimekamilika.

Utekelezaji wa mradi huo pia unahusisha miundombinu ya waenda kwa miguu na njia za waendesha baiskeli pamoja na ujenzi wa kituo cha mabasi ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka (BRT).