Watoto wafundishwe kusoma vitabuWatoto wafundishwe kusoma vitabu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema uandishi wa vitabu una mchango mkubwa katika kuhifadhi utamaduni wa taifa na kujenga uzalendo kwa watoto kupitia vitabu vinavyoakisi maadili na mila za Kitanzania.

Akizungumza Februari 17, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa vitabu vya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Mkenda amewahimizia waandishi, hasa wa vitabu vya watoto, kuandika kazi zitakazowasaidia watoto kujitambua, kuthamini utamaduni wao na kukua wakiwa wazalendo

Amebainisha kuwa licha ya umuhimu wake kwa maendeleo ya taifa, sekta ya uandishi wa vitabu bado haijapewa kipaumbele cha kutosha. Hata hivyo, aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili vitabu vichapishwe, vinunuliwe na kusambazwa katika shule na maktaba nchini. SOMA: Kumekucha maonesho ya vitabu Dar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *