Baada ya kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa maji safi na salama kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Salama Dar es Salaam (DAWASA), Wakazi wa kata ya Sumi iliyopo manispaa ya Ubungo wameanza kuandikishwa ili kufungiwa huduma hiyo kwenye nyumba zao kufuatia kufika ukingoni kwa mradi wa maji utakaohudumia wakazi zaidi ya 47,000 kata za Msumi A, Msumi B na Msumi C na maeneo jirani.

Mhandisi wa DAWASA wilaya ya Ubungo, Mhandisi Sheka Mussa amesema uandikishaji huo unaendelea vizuri na muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa huku huduma za maji zikitarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *