Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameendelea kuandika historia katika mtandao wa YouTube. Kupitia nyimbo zake ambazo  zimevunja rekodi kwa kupata watazamaji wengi zaidi ndani na nje ya Afrika.

Diamond ambaye ni miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika. Ameendelea kuwa tishio huku akiwapiku mastaa wenzake kutoka Bongo ambao ni Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Nandy na wengineo.

Diamond akiwa na msanii wa DR Congo, Innoss’B kwenye video ya  ‘Yope Remix’

Moja ya nyimbo zake ambazo zimepata wafuatiliaji wengi zaidi ni Yope Remix, aliyoshirikiana na msanii wa DR Congo, Innoss’B. Video ya wimbo huo iliachiwa Septemba 7, 2019 na kuwa gumzo Afrika. 

Diamond akiwa na Harmonize, kwenye video ya wimbo ‘Kwangwaru’, ulioachiwa Aprili 14, 2018.

Ndani ya muda mfupi wimbo huo ulifanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 100, huku ikiweka rekodi ya kuwa miongoni mwa video zilizofikisha watazamaji wengi kwa muda mfupi Afrika Mashariki. Aidha hadi kufikia sasa wimbo huo umetazamwa zaidi ya mara milioni 260 YouTube.

Diamond akiwa na staa wa Congo, Fally Ipupa, aliyemshirikisha wimbo ‘Inama’ 

Mwaka mmoja mbele 2020, kwa mara nyingine Diamond aliendelea kuonesha ukubwa wake.Aliachia kigongo kingine, wimbo uitwao Waah! akimshirikisha gwiji wa muziki kutoka Congo, Koffi Olomidé. 

Video ya wimbo huo iliachiwa Novemba 30, 2020 na kupokelewa kwa kishindo kutokana na ubora na hadhi ya wasanii hao wawili. Waah! imetazamwa zaidi ya mara milioni 190 huku ikikadiriwa kuendelea kukusanya namba kila siku.

Wimbo mwingine ambao umeorodheshwa kutazamwa mara nyingi ni Inama. Ambao Diamond alimshirikisha staa wa Congo, Fally Ipupa. Wimbo huo ulitolewa mwaka 2019 huku ukiwavutia wengi kutokana na mchanganyiko wa dansi, Kiswahili na Kifaransa. Mpaka kufikia sasa, Inama umetazamwa zaidi ya mara milioni 160 kwenye YouTube.

Diamond akiwa na gwiji wa muziki kutoka Congo, Koffi Olomidé ambaye wamefanya pamoja wimbo Waah!

Aidha, wimbo mwingine ni Kwangwaru, uliachiwa Aprili 14, 2018. Ulimkutanisha Diamond na msanii mwenzake kutoka Bongo, Harmonize. Ngoma hiyo ilitawala kwa muda mrefu katika mitandao ya kijamii na redioni, huku video yake ikitazamwa zaidi ya mara milioni 130. Wimbo mwingine ni Nana aliyomshirikisha Mr Flavour umetazamwa mara milioni 110.

Kupitia kazi hizo Diamond ameendelea kuthibitisha ubora wake na nafasi yake kama kinara wa muziki Afrika Mashariki. Huku mtandao wa YouTube ukiendelea kuwa jukwaa muhimu linalompaisha kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *