Wakati wa ziara ya Hadja Lahbib, Kamishna wa Ulaya anayehusika na Usawa, Maandalizi na Usimamizi wa Migogoro jijini Kinshasa, EU imetangaza Jumanne, Februari 17, kutolewa kwa euro milioni 81.2 milioni kama msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa wa mgogoro unaoikumba Kivu Kaskazini na Kusini.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi

Wakati Hadja Lahbib, Kamishna wa Ulaya anayehusika na Usawa, Maandalizi na Usimamizi wa Migogoro, Jumanne, Februari 17 alipokuwa akizuru jijini Kinshasa , Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza euro milioni 81.2 kama msaada wa dharura wa kibinadamu kwa DRC.

“Mgogoro unaoongezeka mashariki mwa DRC kwa sasa unasababisha watu wengi kuhama makazi yao. Rasilimali za chakula, maji, na makazi zimekaribia kuisha, na wanawake na watoto wanazidi kukabiliwa na vurugu na kufanyiwa uhalifu,” EU imeandika katika taarifa yake. Wadau wa masuala ya kibinadamu walioko katika maeneo hayo wanaonya mara kwa mara kwamba hali mashariki mwa DRC imekuwa ikizidi kuwa mbaya tangu mji wa Goma kuanguka mikononi mwa waasi wa M23 mnamo Januari 2025.

Burundi, baada ya DRC na kabla ya Rwanda

Kupitia ufadhili huu mpya, Brussels inakusudia, haswa, kutoa huduma muhimu kwa waathiriwa wa Kongo wa mzozo huko Kivu Kaskazini na Kusini. Kati ya euro milioni 81.2 zilizotengwa, euro milioni 68 zimetengwa kwa ajili ya misaada ya dharura kwa familia zilizokimbia makazi yao na kusaidia huduma za ulinzi, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa manusura wa vurugu na ulinzi wa watoto.

Jumla iliyobaki – takriban euro milioni 13 – imetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wa Kongo katika nchi jirani, haswa Burundi. Mpango wa Mwitikio wa Kibinadamu wa mwaka 2026 kwa DRC unakadiria kuwa dola bilioni 1.4 zinahitajika kuwasaidia watu zaidi ya milioni 7 wanaohitaji msaada huo katika sehemu ya mashariki ya nchi.

DRC ni kituo cha kwanza tu cha ziara ya Kamishna wa Ulaya wa Usawa, Maandalizi na Usimamizi wa Migogoro katika eneo la Maziwa Makuu. Baada ya DRC na kabla ya Rwanda, anatarajiwa nchini Burundi leo Jumatano, Februari 18.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *