Kama ilivyo huko Ukraine, Sudan na kwenye eneo la Sahel, matumizi ya ndege zisizo na rubani yameendelea kuonesha nguvu ya misuli ya mataifa na sasa hivi kwenye eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Umuhimu wa silaha hii, ulionekana zaidi mapema mwezi Februari mwaka jana wakati waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda, kudai kutumia ndege zisizo na rubani kushambulia kituo cha jeshi la Kongo FARDC kilichokuwa kinatumika kuongoza na kurusha ndege nyuki zake mjini Kisangani.

Mji huo ikiwa Katikati yam ji mkuu Kinshasa nae neo la mashariki linalokaliwa na waasi wa M23, uwanja wa ndege wa Kisangani unatumiwa na jeshi la kongo kama kitovu cha kimkakati cha mashambulizi yake ya ndege zisizo na rubani na zile za kivita aina ya Sukoi dhidi ya waasi hao.

Pande hasimu kwenye mzozo wa mashariki ya DRC zimekuwa zikiripotiwa kutumia droni ambazo zimesababisha vifo vya raia.
Pande hasimu kwenye mzozo wa mashariki ya DRC zimekuwa zikiripotiwa kutumia droni ambazo zimesababisha vifo vya raia. AP – Moses Sawasawa

Kutokana na uwezo wake pamoja na mafunzo wanayopokea kutoka Rwanda, waasi hao wamefanikiwa pakubwa kuchukua maeneo ya mashariki tangu walipoanzisha tena uasi mwaka 2021, uwezo huu ukiwafanya waudhibiti mji wa Goma na Bukavu mwaka jana.

Hata hivyo, jeshi la Serikali kwa upande wake, limefanikiwa pakubwa kudhibiti anga ya nchi hiyo kwa kununua ndege nyuki za kisasa zenye uweze wa Kwenda masafa marefu kutoka China na Uturuki.

Serikali ya DRC imekuwa ikipambana na waasi wa M23 na makundi mengine yenye silaha mashariki ya nchi.
Serikali ya DRC imekuwa ikipambana na waasi wa M23 na makundi mengine yenye silaha mashariki ya nchi. AFP – JOSPIN MWISHA

Vita kati ya waasi hawa na serikali ya Kongo, kila uchao imeendelea kuchukua sura mpya, ambapo Rwanda imetuma mpakani mwa Congo mitambo ya kutatiza rada, mitambo ambayo umoja wa Mataifa unasema inatatiza pia ndege za abiria.

Mzozo wa mashariki mwa Congo, pia unashuhudia uwepo wa mamluki wa kigeni wanaopigana sambamba na jeshi la Serikali, hali ambayo inaufanya mzozo huo kuwa mgumu zaidi kuutatua licha ya makubaliano yam waka jana kati ya Kigali na Kinshasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *