#HABARI: Serikali imetoa ithibati kwa kitabu cha “Dunia Yangu Bora” ili kianze kutumika rasmi kama kitabu cha ziada cha stadi za maisha katika halmashauri 76 ndani ya mikoa 10 nchini.

Mkuu wa Idara ya Miradi wa shirika la CAMFED, Bi. Dominica Lyambo, ameeleza kuwa mpango huo unalenga kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujitambua, kuimarisha nidhamu, na kuongeza ufaulu.

Kupitia mafunzo kwa walimu wa ushauri na unasihi, kitabu hicho kitawasaidia vijana kukabiliana na changamoto za rika, kulinda maadili ya Kitanzania, na kuzuia mimba za utotoni kuelekea lengo la kufikia asilimia 85 ya halmashauri zote nchini ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesisitiza kuwa kitabu hicho ni nyenzo muhimu ya kumjenga kijana mwadilifu, mwaminifu, na mwenye kujali mazingira.

Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu, Dkt. Gladness Kirei, amezitaka halmashauri husika kuweka mipango kazi madhubuti na kuwashirikisha wazazi ili kuleta mabadiliko ya kweli katika tabia za vijana.

Mafanikio ya mradi huu hayatapimwa kwa idadi ya vitabu pekee, bali kwa mabadiliko ya utu, kupungua kwa utoro shuleni, na ongezeko la matendo mema yenye utu miongoni mwa wanafunzi wa kike na wa kiume.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *