#HABARI: Tanzania imepata mafanikio makubwa katika sekta ya nishati baada ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kuongezeka mara tatu, kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 23.2 mwaka 2025.

Akizungumza jijini Paris katika mdahalo wa Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA), Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amebainisha kuwa hatua hiyo inachagizwa na Mkakati wa Kitaifa wa 2024–2034 uliozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kulinda afya, mazingira, na kukuza uchumi.

Katika mwaka huu wa fedha, Serikali imepanga kusambaza majiko banifu 200,000 na mitungi ya gesi 450,000 kwa ruzuku, huku ikianzisha mfumo wa kulipia vifaa vya kupikia umeme kupitia bili za TANESCO ili kupunguza gharama kwa mwananchi.

Aidha, juhudi hizo zinaenda sambamba na amri ya kupiga marufuku matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi kubwa zinazohudumia zaidi ya watu 100, kama shule na hospitali, ili kukabiliana na uharibifu wa misitu na moshi hatarishi wa ndani.

Waziri Ndejembi amesisitiza kuwa mafanikio hayo sasa yanaelekezwa zaidi maeneo ya vijijini ili kupunguza utegemezi wa kuni, huku sekta hiyo ikichukuliwa kama fursa mpya ya kuzalisha ajira.

Tanzania inaendelea kushirikiana na wadau wa kimataifa kuhakikisha malengo ya nishati safi yanafanikiwa kwa uendelevu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kufikia lengo la Afrika la upatikanaji wa nishati safi kwa wote ifikapo mwaka 2040.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *