#HABARI: Wakati akikusanya vitu vyake ili kuondoka Mahakamani Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu alimuona dada yake Mchungaji Rose Masesa akamsisitiza kusali kwa bidii akimuombea.

“Pray hard,” alisema Lissu.
Huku dada yake akiwa kwenye tabasamu akamjibu kuwa anasali kwa bidii.

Kesi ya uhaini Na. 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imeendelea tena leo, Jumatano Februari 18.2026, kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo ya jinai inayosikilizwa mfululizo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru imekuja kwa ajili ya upande wa Jamhuri kuendelea kuwaleta Mahakamani mashahidi na kutoa ushahidi wao.

Ikumbukwe kuwa Jamhuri kwenye kesi hii ina mashahidi 30 na vielelezo tisa (9) kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa Mahakamani hapo siku za nyuma, ambapo kati ya mashahidi hao 30, mashahidi 11 ni wa kificho (siri), yaani raia waliopatiwa ulinzi wa utambulisho wao na Mahakama, na mashahidi waliosalia wote si wa kificho ambao kimsingi ni askari kutoka vyombo mbalimbali vya Ulinzi na Usalama Nchini wengi wao wakiwa ni Maafisa wa Jeshi la Polisi.

Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *