#HABARI: Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya kuangukiwa na ukuta wa jengo la Kanisa, kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Miongoni mwa waliofariki ni mwanamke aliyefahamika kwa jina la Grory Josephat, mkazi wa Kilimahewa, ambaye inadaiwa alikuwa na ujauzito wa takribani miezi sita hadi saba wakati umauti ulipomkuta, huku Mume wa marehemu Aram Elisha, amesema hakutarajia kumpoteza mke wake katika mazingira ya ghafla kiasi hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea wakati waumini walipokuwa wakifanya mazoezi ya kwaya ndani ya kanisa hilo, ambapo ghafla ukuta uliporomoka kutokana na mvua kubwa na upepo mkali.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph, amefika eneo la tukio kutoa pole kwa familia za marehemu pamoja na majeruhi, huku akitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari zaidi wakati huu wa msimu wa mvua.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.
Powered by MCHEZOSUPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *