#HABARI: Zaidi ya wanafunzi 13,000 waliokatisha masomo ya sekondari nchini wamefanikiwa kurejea shuleni kupitia mradi wa SEQUIP-AEP, unaotekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikiana na TAMISEMI.
Mkuu wa taasisi hiyo, Prof. Philipo Sanga, amebainisha kuwa mradi umevuka lengo la awali la wanafunzi 12,000, huku ujenzi wa miundombinu kama mabweni na vyumba vya mama na mtoto ukisaidia kupunguza vikwazo vya kijamii na kiuchumi vilivyokuwa vikiwakabili vijana hao, hususan wasichana.
Meneja wa TEWW Ruvuma, Hellen Lyamuya, ameeleza kuwa utoaji wa elimu ya ujasiriamali umewajengea wanafunzi hao uwezo wa kujiamini na kujitegemea kimaisha.
Aidha, wakufunzi wamebainisha kuwa wanafunzi waliorejea kupitia mfumo huo mbadala wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani ya taifa, hatua inayothibitisha ubora wa elimu inayotolewa na kufuta dhana potofu kuhusu mifumo ya elimu mbadala nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.