
Mwezi mmoja baada ya waasi wa M23/AFC kuondoka kwenye mji wa Uvira jimboni Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC, maisha ya kawaida yameanza kurejea taratibu, huku utawala wa Kinshasa ukirejea.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Viongozi wa serikali wameanza kurejea, wakiwemo maafisa wa polisi katika mjio huo wa upili kwa ukubwa katika jimbo la Kivu Kusini.
Gavana wa jimbo la Kivu Kusini Jean-Jacques Purusi, aliyekuwa amekimbilia jijini Bujumbura nchini Burundi, naye pia amerejea na kuwahimiza wakaazi wa mji huo kurejelea maisha yao ya kawaida.
Licha ya kurejea na hajakwenda kwenye ofisi yake, na katika kikao na wakuu wa usalama, alikutana nao katika makaazi binafsi kwa sababu za kiusalama.
Meya wa Uvira Kifara Kapenda Kiky, ambaye pia alikuwa amekimbia amerejea, lakini majengo ya ofisi yake yamehabiriwa.
Wafanyakazi wengine wa serikali wakiwemo walimu, maafisa wa mahakama bado wamekwama nchini Burundi walikokimbilia, huku nchi hiyo jirani ikiendelea kufunga mpaka wake na DRC na kuendelea kutatiza shughuli za biashara na wananchi wa nchi hizo mbili kutembeleana.