TABORA: SERIKALI imetumia Sh milioni 686 kujenga Ktuo cha Afya cha Nsenda  chenye lengo la kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na wanachi 18,998 kutoka vijji vitano vya kata ya Nsenda.

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Taifa, Kenani Kohongosi alieleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Urambo wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa wilaya hiyo kusikiliza kero zao  jana.

Kihongosi alieleza kuwa CCM imeendelea kusimamia serikali katika utekelezaji wa ilani yake hasa katika siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan madarakani na kuridhishwa na utekelezaji wa ilani hiyo.

Ujenzi wa  kituo icho unatarajia kukamilila ifikapo  Machi 30, 2026  ambapo kwa sasa umefikia asilimia 69.

Mradi wa Kituo Cha Afya Nsenda ulipokea jumla ya Sh milioni  686 ambazo ni fedha kutoka Serikali Kuu, ukihusisha ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la Maabara, Jengo la Mama na mtoto Jengo la kufulia, Vyoo vya nje Pamoja na Kichomea taka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *