
Nchini Msumbiji, kamanda wa zamani wa polisi Bernardino Rafael na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Pascoal Ronda wamehojiwa siku ya Jumanne, Februari 17, na Mwanasheria Mkuu. Kesi hii ni sehemu ya malalamiko yaliyowasilishwa mwezi Aprili na jukwaa la Decide. Shirika hili la kiraia linawashutumu kwa kuhusika na vifo na ukiukwaji wa haki za binadamu uliotokea wakati wa mgogoro wa baada ya uchaguzi kati ya mwezi Oktoba 2024 na Machi 2025. Hii ni mara ya pili wawili hao kuhojiwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix
Kikao cha kusikilizwa kwa watuhumixwa hao kilichukuwa muda mfupi. Bernardino Rafael na Pascoal Ronda walitumia chini ya saa moja katika ofisi ya mwendesha mashtaka. “Hilo ni jambo la kawaida,” chanzo kilicho karibu na kesi hiyo kimekiri. “Ilikuwa hasa kuwafahamisha hatua zinazofuata.” Mwendesha mashtaka tayari amefanya vikao kadhaa. Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, maafisa katika makao makuu ya polisi, na maafisa wa polisi huko Maputo na katika mikoa yote ya nchi walihojiwa.
Sasa ni zamu ya familia za waathiriwa, manusura, na wanachama wa mashirika ya kiraia. Kufuatia hili, mwendesha mashtaka ataamua kama aendelee na kesi au la. “Nina imani kubwa. Kesi inajengwa katika mwelekeo huo,” anasema Wilker Dias, mratibu wa jukwaa la Decide. Ingawa shirika hilo mara nyingi limekuwa likilaani ukosefu wa uhuru wa mahakama ya Msumbiji, bado ana matumaini. “Hii ni fursa ya kipekee ya kuthibitisha kwamba mfumo wetu wa mahakama unaweza kufanya kazi,” ameongeza. “Haki ni hatua isiotengana kwa maridhiano.”
Tangu mwezi Oktoba, Msumbiji imeanzisha mazungumzo makubwa ya kitaifa. Kulingana na mashirika ya kiraia, mgogoro wa baada ya uchaguzi ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 500.