ARUSHA: VIJANA nchini wametakiwa kutumia bunifu ili waweze kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kupitia biashara mbalimbali kupitia mashirika binafsi na serikali kwa ujumla
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuwawezesha vijana ya Save Youth Dreams Foundation (SYDF) Dk, Gloria Mheta wakati akizungumza mbele ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dk Fred Msemwa , Uongozi wa Chuo Cha Elimu yahara( CBE ),Wadau wa masuala ya uwekezaji na uchumi pamoja na wanafunzi wa CBE alipohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa klabu ya vijana inayoitwa (Youth Investment Club) kampasi kuu ya Dar es salaam.
Amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia mbinu mbalimbali za uwekezaji kujikwamua kiuchumi ili waweze kufanikiwa kimaisha huku akisisitiza lengo la kuanzisha klabu hiyo ni kuwawezesha vijana hasa wanafunzi kupata elimu sahihi ya matumizi ya fedha , uwekezaji na fursa zilizopo zinazotolewa na serikali na mashirika binafsi.

Naye Dk , Msemwa amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuwawezesha vijana hasa wanafunzi wa elimu ya juu kwenye masuala ya fedha, uwekezaji, ujasiriamali, teknolojia na uvumbuzi ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia bunifu mbalimbali kupitia mashirika binafsi na serikali ili waweze kujiajiri
“Kupitia bunifu tunaona fursa mbalimbali za kiuchumi hivyo serikali itashirikiana na mashirika mbalimbali katika kukuza uchumi na bunifu kupitia klabu mbalimbali zinazoanzishwa pamoja na mashirika yanayotoa fursa kwa vijana kujikwamua kiuchumi”

Huku Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi kuu y Dar es Salaam , Profess Edda Lwoga akisema uzinduzi wa klabu hiyo utawezesha wanafunzi kutumia fursa za mafunzo yanayotolewa chuoni hapo yatakayowasaidia vijana kujiajiri kwa kuwa wawekezaki, wafanyabiashara na wajasiriamali ili kuondokana na changamoto za ajira nchin