TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 17, 2026 imekutana na Mwanasheria Andrew Chenge kwa ajili ya kupata maoni na ushauri wake.

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika, uliopo katika jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam, ukiwa sehemu ya mchakato wa Tume kukusanya taarifa kutoka kwa viongozi na wadau mbalimbali wa kitaifa. SOMA: Tume Yakutana Mwamunyange,Waitara

Katika mazungumzo hayo, wajumbe wa Tume na Mwanasheria Chenge walijadili tathmini ya athari za matukio ya uvunjifu wa amani ndani na nje ya nchi pamoja na hatua za kijamii na kisheria zinazoweza kuchukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano na utulivu wa taifa.

Tume hiyo inaendelea na mikutano na makundi mbalimbali, ikiwemo waathirika wa matukio hayo kwa lengo la kukusanya ushahidi na maoni yatakayosaidia kuandaa ripoti ya kina itakayotoa mapendekezo ya kudumisha amani na kuzuia matukio kama hayo siku zijazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *