Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico ameonya kwamba Umoja wa Ulaya (EU) sasa hivi unakabiliwa na hali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia yake, huku matatizo ya kiuchumi yakizidishwa na kukosekana uongozi na maono ya muda mrefu huko Brussels.

Fico ametoa matamshi alipohutubia mkutano wa kujadili nyumba za kukodisha za bei nafuu katika mji mkuu wa nchi hiyo Bratislava, na kueleza kwamba matatizo na magumu yanayowakabili watu wa kawaida wa Ulaya ni sehemu ya unyong’onyevu ulioiathiri kambi nzima ya EU.

“Umoja wa Ulaya haujawahi kuwa katika hali mbaya kama hii uliyonayo hivi sasa,” ametanabahisha rais huyo wa Slovakia, akiongeza kuwa, hali hiyo “haihusu tu viashiria vya kiuchumi, bali inahusiana pia na uongozi na maono.”

Ameendelea kutahadharisha kwa kusema, bila ya kuwa na mkakati thabiti kuhusiana na ushindani, EU inaweza “kugeuka jumba la wazi la makumbusho ya kiutamaduni,” na kuwa hatarini kushuka zaidi katika jukwaa la kimataifa.

Fico amebainisha kuwa, baadhi ya maeneo ya dunia, kama vile China, sasa hivi yako mbele zaidi ya EU kwa miaka 15-20 katika sekta muhimu.

Rais wa Slovakia amekuwa akiukosoa mara kwa mara Umoja wa Ulaya kuhusiana na sera zake, hususan kuhusu nishati na vikwazo dhidi ya Russia, akisema vikwazo hivyo “vinaiumiza” kambi hiyo tu. 

Fico, ambaye mwaka 2024 alinusurika jaribio la mauaji lililofanywa na mwanaharakati anayeiunga mkono Ukraine, ameielezea Kiev kama “shimo jeusi” la ufisadi ambalo limemeza mabilioni ya yuro katika fedha za EU. Mwezi uliopita, alitoa wito wa kuondolewa mkuu wa sera za nje wa umoja huo Kaja Kallas, anayejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya Russia…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *