
Nchini Afrika Kusini, Kaimu Waziri wa Polisi amebainisha Bungeni siku ya Jumanne, Februari 17, kutumwa kwa jeshi ndani ya siku kumi kupambana na uhalifu, hasa vurugu za magenge. Hatua hii, iliyotajwa Februari 12 na Rais Cyril Ramaphosa katika hotuba yake kwa taifa, imeibua maswali mengi miongoni mwa wanasiasa na wataalamu wa masuala ya ulinzi. Kwa miaka kadhaa, jeshi limekuwa likitumika zaidi kufidia mapungufu katika jeshi la polisi.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Idadi ya wanajeshi ambao Afrika Kusini itawatuma kupambana na uhalifu na magenge bado haijulikani. Lakini kulingana na Waziri wa Polisi Firoz Cachalia, maeneo matatu yaliyoathiriwa hasa na uhalifu yatalengwa: jimbo la Western Cape, ikiwa ni pamoja na Cape Town; jimbo la Gauteng, amako kunapatikana miji ya Johannesburg na Pretoria; na hasa jimbo la Eastern Cape, ambapo uhalifu unaohusiana na magenge umeongezeka sana katika miji kama Port Elizabeth, pamoja na East London na Mthata.
Kwa kupelekwa huku kwa jeshi, serikali inasema inataka kuwasaidia polisi, ambao wamezidiwa na vurugu za magenge na uchimbaji madini haramu. Afrika Kusini ina mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya vifo duniani: takriban vifo 60 kwa siku, baadhi vikihusishwa na makabiliano kati ya magenge kwa minajili ya kudhibiti maeneo ya kuuza dawa za kulevya, hasa Cape Town, au mauaji unaohusiana na uchimbaji madini haramu katika jimbo la Gauteng.
Mnamo mwaka 2019, jeshi liliitwa kushughulikia magenge ya Cape Town… bila mafanikio ya kudumu.
Tangazo la serikali limepokelewa kwa tahadhari na baadhi ya vyama vya siasa, anasema mwandishi wetu huko Johannesburg, Josephine Kloeckner. Mmusi Maimane, kiongozi wa chama cha BOSA, alisema: “Kupeleka jeshi hakuwezi kuwa suluhisho la kudumu kwa tatizo sugu la uhalifu. Askari si maafisa wa polisi. Kwa hivyo nadhani kupeleka jeshi hili lazima kuwe hatua ya muda, na jambo muhimu zaidi ni kuimarisha uwezo wa jeshi la polisi.”
Kwa waangalizi wengi, uamuzi huu ni kukiri kushindwa kwa polisi. Jeshi linazidi kuitwa kuunga mkono polisi. Mwelekeo huu unamtia wasiwasi Ricardo Teixeira, mtaalamu wa msuala ya usalama: “Hili haliko ndani ya mamlaka ya vikosi vya jeshi, na hawajafunzwa kuingiliana na raia.” Huu ni mzigo wa ziada wa kifedha kwa jeshi, ambao haliwezi kuubeba na ambao unatokana na bajeti ambayo tayari haitoshi.”
Mtafiti John Stupart pia anaelezea mashaka, kwani vikosi vya jeshi vya Afrika Kusini vyenyewe vimezidiwa na shughuli nyingi, havina ufadhili wa kutosha, na havina mafunzo ya kupambana na uhalifu. Mnamo mwaka 2019, jeshi hilo lilitumwa kupambana na magenge huko Cape Town, bila mafanikio ya kudumu. Mbali na hayo, jeshi la Afrika Kusini linapitia kipindi cha kutafakari na kurekebisha kufuatia tangazo la kujiondoa kwake kutoka MONUSCO nchini DRC mapema mwezi Februari, ambapo lilikuwa sehemu ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kwa miaka 27.