Ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hii na mafanikio yaliyofikiwa hadi kufikia sasa, Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa amemtembelea Profesa Barbara Batte, Mkufunzi anayefundisha lugha ya Kiswahili, yeye na wenzake katika Chuo Kikuu cha Havana na katika Nyumba ya Afrika nchini Cuba.
Takribani miaka 43 iliyopita, Barbara Batte Guevara, alijifunza kwa muda mfupi lugha ya Kiswahili nchini Tanzania lakini mbegu hiyo iliyopandwa karibia nusu karne iliyopita, anataka aipande kwa Wacuba wengine ili ichipue na kuzaa miche zaidi ya lugha ya Kiswahili kote Cuba, ukanda wa Karibiani na hata kote Amerika.