
Mataifa ya Uingereza, Canada na Umoja wa Ulaya, yamelaani vita vinavyoendelea nchini Sudan kwa karibu miaka mitatu sasa na kusema, kinachoendelea ni uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katia taarifa ya pamoja, mataifa hayo ya Magharibi yanataka uchunguzi huru na wa haraka, kufanyika nchini Sudan na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika kuchukua hatua.
Vita kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF wanaotafuta udhibiti na utawala wa nchi hiyo, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine zaidia ya Milioni 11 wameyakimbia makaazi yao.
Nchi hizo, zimelaani mateso dhidi ya raia wa kawaida, hasa wanawake na watoto ambayo wamesema yanakwenda kinyume na sheria za kimataifa.
Taarifa hiyo pia imelaani ripoti za ubakaji wa wasichana na wanawake, katikati ya mzozo ambao umesababisha ukame ambao umeleta njaa kubwa katika taifa hilo tangu kuanza vita mwaka 2023.