Gesi asilia imeendelea kutajwa kuwa nguzo muhimu ya ukuaji wa uchumi wa taifa kutokana na uwezo wake wa kutoa nishati nafuu, ya uhakika na rafiki kwa mazingira.

Matumizi ya nishati hiyo yameelezwa kupunguza gharama za uzalishaji katika viwanda na sekta nyingine za kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kuongeza tija katika shughuli za maendeleo. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imesema hayo wakati ilipotembelea kituo mama cha kushindilia gesi asilia cha Mlimani-CNG jijini Dar es Salaam, kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

#AzamTVUpdates
✍Theresia Mbembela
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *