#HABARI: Baraza la Madiwani la Manispaa ya Temeke limepitisha rasimu ya bajeti ya Shilingi bilioni 192.6 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2026/27, ambapo Shilingi bilioni 75 zinatarajiwa kutokana na makusanyo ya ndani na bilioni 98 ikiwa ni ruzuku kutoka Serikali Kuu.
Mstahiki Meya wa Temeke, Uzairu Abdul Athumani, amebainisha kuwa asilimia 70 ya bajeti hiyo imeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, na miundombinu ya barabara, huku akiwahimiza wananchi kulipa kodi kwa uaminifu ili kufikia malengo hayo.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbagala, Abdulkarim Pazi, ameeleza kuwa bajeti hiyo inakidhi matarajio ya wananchi kutokana na kutoa kipaumbele katika maboresho ya miundombinu kwenye kata mbalimbali.
Hatua hii inalenga kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii ndani ya manispaa hiyo, huku uongozi ukijipanga kuhakikisha fedha zilizotengwa zinatekeleza miradi ya kipaumbele kwa ufanisi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania