#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Subira Mgalu, imetoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) ili kukidhi mahitaji yanayokua nchini.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo katika kituo cha CNG Mlimani, Mhe. Mgalu alibainisha kuwa matumizi ya CNG yanapunguza gharama za usafiri kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mafuta, huku akiishauri Serikali kuharakisha ufungaji wa mifumo hiyo kwenye magari yake ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema Serikali tayari imeanza kutumia mfumo wa CNG kwenye mabasi mapya ya mwendo kasi na imeshaagiza magari makubwa matano ya kusambaza gesi hiyo katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Arusha, na Tanga.
Aidha, Kamati imepongeza jitihada za Wizara ya Nishati na TPDC ambazo zimepelekea zaidi ya vyombo vya usafiri 15,000 kutumia nishati hiyo, huku ikihimiza uendelezaji wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania