#HABARI: Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio, amekutana na uongozi wa Benki ya NBC jijini Dodoma kujadili ushirikiano wa kuwawezesha wawekezaji wazawa.
Dkt. Mataragio ameipongeza benki hiyo kwa utayari wake wa kutoa mitaji wezeshi, akibainisha kuwa ushirikiano huo utasaidia wadau wa ndani kumudu uwekezaji katika miradi ya mafuta na gesi ambayo mara nyingi hukwama kwa kukosa fedha.
Dkt. Mataragio amesisitiza kuwa Serikali inatamani kuona wawekezaji wazawa wakijenga viwanda na kuanzisha biashara zitakazozalisha ajira kwa vijana na kukuza mchango wa sekta ya nishati katika uchumi wa taifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa NBC anayeshughulikia wateja wakubwa na Serikali, Bw. Elvis Ndunguru, amethibitisha utayari wa benki hiyo kutoa mikopo kwa wawekezaji wa kila ngazi ili kufikia malengo ya Serikali ya kuimarisha uwekezaji wa ndani.
Kutokana na kikao hicho, Wizara ya Nishati na NBC zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa vikwazo vya kifedha vinavyowakabili Watanzania wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta hiyo.
Ushirikiano huu unatarajiwa kuleta matokeo chanya kwa kuchochea ukuaji wa viwanda, kutengeneza fursa mpya za kazi, na kuboresha maisha ya wananchi kupitia nishati endelevu na maendeleo ya kiuchumi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania