#HABARI: Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, imeendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Katika muendelezo wa kesi hiyo upande wa Jamhuri umeendelea kuwasilisha mashahidi wake, akianza na Askari Polisi Mpelelezi, Detective Koplo Vicent, aliyetoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Ignas Mwinuka.
Shahidi wa 13 wa Jamhuri, ambaye ni shahidi wa siri aliyepewa utambulisho wa P3, ametoa ushahidi wake akieleza kuwa yeye ni mkazi wa Mbeya na dereva bodaboda mwenye umri wa miaka 35.
Shahidi huyo ameiambia mahakama kuwa amekuwa mfuasi wa CHADEMA tangu mwaka 2021 na amekuwa akishiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za chama hicho mkoani Mbeya, ikiwemo mikutano na maandamano ya kisiasa.
Katika ushahidi wake, P3 amekumbusha ushiriki wake kwenye maandamano ya chama hicho mkoani Mbeya mwaka 2024 yaliyoongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe.
Aidha, amegusia tukio la kongamano la vijana (BAVICHA) lililopaswa kufanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ruanda-Nzovwe mkoani humo, ambalo hata hivyo halikufanyika baada ya serikali kuzuia mkusanyiko huo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania