#HABARI: Mahakama Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali maombi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika majimbo nane ya kisiwani Pemba, yaliyokuwa yamewasilishwa na wagombea kutoka Chama cha ACT-Wazalendo.

Jaji Haji Khamis Suleiman alitoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na pingamizi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, zilizobainisha kuwa maombi hayo yalikuwa na kasoro nyingi za kisheria ambazo zilizuia mahakama kuendelea na shauri hilo.

Sababu kuu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kasoro za kisheria zilizobainika kwenye hati za kiapo (affidavits) ambazo waombaji waliziwasilisha kama sehemu ya uthibitisho wao.

Mahakama ilijiridhisha kuwa kutokana na mapungufu hayo, hati hizo haziwezi kutambuliwa kisheria, jambo lililopelekea kufutwa kwa mashauri hayo ya majimbo ya Kiwani, Mkoani, Chake Chake, Chonga, Wawi, Wingwi, Micheweni, na Kojani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *