#HABARI: Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wamejitokeza kuifariji familia ya aliyekuwa Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay, kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Mariana Tkuway, aliyefariki dunia Februari 14, 2026.
Marehemu Mariana, aliyekuwa akiumwa tangu mwaka 2019, ameelezwa na jamii kama mlezi na mshauri mwema aliyeacha alama kubwa ya maadili na malezi bora kwa familia na jamii nzima kwa ujumla.
Katika maombolezo hayo, aliyekuwa mbunge Flatei Massay amewashukuru wananchi kwa mshikamano na upendo mkubwa waliouonyesha, akibainisha kuwa umoja huo unaipa familia faraja katika kipindi hiki kigumu.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu, ametoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali akihimiza jamii kuendelea kudumisha utamaduni wa kusaidiana na kupendana wakati wa shida na raha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania