#HABARI: Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imekanusha dhana kuwa uwekezaji ni kwa ajili ya wawekezaji wa nje pekee, ikisisitiza kuwa kipaumbele chao kikubwa ni kuona Watanzania wakifanya uwekezaji wenye tija ndani ya nchi.
Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji wa TISEZA, Bw. Daudi Riganda, ameyasema hayo wilayani Mbozi baada ya kutembelea viwanda vya wawekezaji wa ndani vinavyochakata kahawa na parachichi, ambavyo tayari vimeanza kunufaika na fursa na vivutio vinavyotolewa na mamlaka hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bw. Jabir Makame, ameipongeza TISEZA kwa kuhamasisha uwekezaji na kubainisha kuwa mkoa wake umetenga maeneo 16 yenye ukubwa wa ekari 4,204 kwa ajili ya ujenzi wa kongani za viwanda.
Bw. Makame amesisitiza kuwa Songwe ina fursa lukuki katika sekta za kilimo, madini, na ufugaji, na amewakaribisha wawekezaji kutumia maeneo hayo yaliyotengwa ili kuongeza thamani ya mazao na kukuza uchumi wa mkoa na taifa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania