#HABARI: Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano katika Mtaa wa Vikawe, Kibaha mkoani Pwani, umeanza kupatiwa utatuzi baada ya wananchi na mmiliki wa eneo kufikia maridhiano ya kulipia Shilingi 3,000 kwa kila mita moja ya mraba.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya majadiliano ya saa tatu na uongozi wa wilaya, ambapo sasa zoezi la upimaji linaruhusiwa kuanza ili kuwawezesha wakazi zaidi ya 1,600 kupata umiliki halali wa maeneo yao.

Licha ya hatua hiyo kuleta matumaini mapya, viongozi wa kamati za wananchi wametoa angalizo kwa serikali kuwa makini wakati wa zoezi la upimaji ili kulinda haki za kila mkazi.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bwana Nickson Simon, amewahimiza wananchi kushirikiana kikamilifu katika mchakato huo wa utatuzi ili kumaliza kabisa mivutano ya muda mrefu na kuchochea maendeleo katika Kata ya Pangani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *