#HABARI: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Serikali kwa usimamizi madhubuti wa mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja (BPS) unaohakikisha nishati hiyo inapatikana kwa wakati na uwazi.
Akizungumza baada ya kutembelea miundombinu ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kigamboni, na Kurasini, Mhe. Mgalu amebainisha kuwa mfumo huo unalinda maslahi ya taifa kwa kutoa takwimu sahihi za mafuta yanayoingia nchini na kuwezesha ukusanyaji wa tozo mbalimbali kwa uaminifu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesisitiza kuwa mfumo huo umeongeza uaminifu kwa nchi jirani na kwa sasa nchi ina akiba ya kutosha ya aina zote za mafuta.
Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Erasto Simon, ameongeza kuwa mfumo huo umewezesha ukusanyaji wa kodi kwa asilimia 100, ambapo kwa sasa Mamlaka ya Mapato (TRA) inaweza kukadiria mapato yatakayopatikana miezi miwili kabla kutokana na mpangilio mzuri wa zabuni za uagizaji.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania