Huwezi kutaja historia ya nishati nchini Tanzania bila kuitaja Hale Hydroelectric Power Station. Hiki ni kituo cha Pili kujengwa cha kuzalisha umeme wa maji nchini baada ya kile cha Pangani. Ujenzi wa kituo hiki ulianza mwishoni mwa miaka ya 1950 na kilianza rasmi uzalishaji wa umeme mwaka 1964.
Kutokana na kudumu kwake kwa muda mrefu, miundombinu na mitambo yake ilianza kuzeeka na kuhitaji maboresho makubwa ili kuendana na mahitaji ya sasa ya nishati.
Ndipo Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ikaamua kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji mkubwa wa kituo hicho. Maboresho hayo yamelenga kuongeza ufanisi wa uzalishaji, kuimarisha usalama wa mitambo, na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Mbali na kuongeza uwezo wa uzalishaji, mradi wa ukarabati umeleta manufaa kwa jamii inayozunguka eneo hilo kupitia ajira mbalimbali zilizochochea kipato cha wananchi na kukuza uchumi wa eneo husika.
(Feed generated with FetchRSS)