Kilimanjaro. Kampuni ya Mawasiliano Tanzania Yas leo imekabidhi hundi ya Sh5 milioni kwa mkazi wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Petro Mefurda ambaye ameibuka mshindi wa droo ya tatu ya kampeni inayoendelea.

Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika mjini Moshi, Meneja wa Duka la Yas Moshi, Francis Joseph, alisema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya kampuni kuwashukuru wateja wake kwa kuendelea kuichagua kampuni hio katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kubadilika kwa chapa.

Joseph alibainisha kuwa kampeni ya Tunasheherekea Pamoja – Mwaka Mmoja wa Yas imebuniwa kuleta fursa kwa watumiaji wa huduma za Yas kujishindia zawadi mbalimbali zenye lengo la kuongeza thamani katika maisha yao. “Tunatambua mchango wa wateja wetu katika safari ya Yas. Ndiyo maana tunawazadia wateja wetu kwa namna itakayowawezesha kwenye shughuli zao mbalimbali,” alisema.

Kwa upande wake, mshindi Petro Mefurda, akielezea namna anavyopanga kutumia zawadi hiyo ya Sh5 milioni, alisema ushindi huo umekuja katika kipindi sahihi na utasaidia kuongeza mtaji ili kuboresha shughuli zake za kijamii na kiuchumi. “Sikutarajia kabisa, lakini Yas wamethibitisha kuwa Kampeni zao ni halali na zenye manufaa kwa jamii. Nawashauri wateja wa Yas kuendelea kushiriki ili nao waweze kushinda,” alisema Mefurda.

Kampeni hio inaendelea kote nchini na wateja wote wa Yas wanahimizwa kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo ili kujipatia nafasi ya kushinda zawadi za kila siku, wiki, pamoja na zawadi kuu ya Sh100 milioni mwishoni mwa kampeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *