Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Waziri Rajab Salum amezitaka taasisi zinazosimamia sekta ya viwanda na biashara kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia wajasiriamali wabunifu kupata mikopo na mitaji ya kifedha ili waweze kuanzisha na kuendeleza viwanda na biashara zao.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya katika Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO), Balozi Waziri amesema mitaji ni msingi wa maendeleo ya viwanda vya ndani na ushindani wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *