.

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani inajiandaa kuondoa wanajeshi wake waliosalia kutoka
Syria katika miezi michache ijayo, afisa mkuu wa Ikulu ameiambia BBC.

Afisa huyo alisema serikali ya Syria imekubali kuchukua
uongozi katika kupambana na ugaidi ndani ya mipaka yake na uwepo wa kijeshi wa
Marekani “kwa kiwango kikubwa” hauhitajiki tena.

Wanajeshi wa Marekani wamekuwa Syria tangu mwaka 2015, kama
sehemu ya kampeni ya kupambana na ugaidi ili kukabiliana na ushawishi wa Dola
la Kiislamu (ISIS).

Uamuzi huo umekuja huku Rais wa Marekani Donald Trump
akiongeza uwepo wake wa kijeshi Mashariki ya Kati huku mvutano na Iran
ukiongezeka.

Afisa huyo alibainisha kuwa uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi
takriban 1,000 waliosalia Syria ni sehemu ya mpito unaozingatia masharti, na
kwamba Marekani bado iko tayari kujibu vitisho vyovyote katika eneo hilo.

Habari hizo – zilizoripotiwa kwa mara ya kwanza na Wall
Street Journal – zinakuja huku kukiwa na ongezeko la wanajeshi wa Marekani eneo
la Mashariki ya Kati, hasa karibu na Iran.

BBC Verify imethibitisha eneo la meli ya Marekani ya USS
Abraham Lincoln – ikiwa na makombora na ndege kadhaa za kivita – karibu na
Iran.

Marekani pia imeripotiwa kutuma meli ya USS Gerald R Ford,
meli kubwa zaidi ya kivita duniani, Mashariki ya Kati, inayotarajiwa kuwasili
katika eneo hilo ndani ya wiki tatu zijazo.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *