
Wakazi na wafanyabiashara wa Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),wanaomba mpaka na Burundi ufuguliwe tena. Mwezi mmoja baada ya waasi wa AFC/M23 kuondoka katika mji wa Uvira, milio ya risasi imekoma, haisikike tena, lakini mpaka bado umefungwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi anakumbusha kwamba hali ya usalama bado haijawa sawa ili mpaka wa nchi yake na DRC uweze kufuguliwa tena.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko Uvira, Florence Morice
Wakazi wa mji wa Uvira na vitongoji vyake wamemuomba Gavana wa mkoa wa Kivu Kusini Jean-Jacques Purusi kufanya liliyo chini ya uwezo wake mpaka na Burundi ufunguliwe.
Katika mlango wa soko la Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), muuzaji mmoja anamuomba gavana wa mkoa wa Kivu Kusini kufanya kinachowezekana mpaka huo ufunguliwe tena. “Fungueni mpaka,” anasema, mbele ya vibanda vyenye watu wachache. Tangu kufungwa kwa mpaka huo, uchumi wa eneo hilo umepungua sana.
Mwanamke mwingine anamkaribia gavana na kumuomba: jamaa zake walikimbia wakati AFC/M23 ilipofika na wameendelea kukwama upande wa Burundi. “Watoto wengi wapo, hata waumini wa kanisa, wote wapo. Kuna watoto wangu na watoto wa mjomba wangu,” anasema.
“Hisia ya kutokuwa na nguvu mbele ya mateso haya”
Gavana Jean-Jacques Purusi anasikiliza na kuelezea kuchanganyikiwa kwake. Kwake, kuna “hisia ya kutokuwa na nguvu mbele ya mateso haya. Tunataka mpaka ufunguliwe haraka iwezekanavyo. Lakini pia kuna mambo muhimu ya usalama yanayohusiana na hali halisi ya nchi zote mbili. Ni muhimu kuelewa kwamba adui hayuko mbali sana. Wako hapa Sange, kilomita 30 kutoka Uvira, na kwenye vilima, wako kama kilomita kumi na tano kutoka hapa.”
Lakini badhi wanaona kuwa na kisingizio tu. Raphaël, 19, alikimbia kambi ya wakimbizi ya Busuma. “Kuna mateso mengi huko. Mateso mengi. Na ukosefu mkubwa wa maji.” Alivuka Ziwa Tanganyika kwa mtumbwi usiku, akihatarisha maisha yake. “Tulikuwa watatu, lakini ndugu zangu walibaki Gatumba kwa sababu walikamatwa.”
Karibu naye, mwanamume mmoja pia anasimulia namna alivyovuka katika mazingira magumu, akishikilia dumu la kawaida ili kuendelea kuelea majini alipokuwa akivuka mto kuelekea DRC. Kulikuwa na kumi na wanne mwanzoni; wawili hawakuweza kufika ufukweni upande wa pili wa mto (DRC)