Vyombo vya habari vya utawala wa kibaguzi wa Israel vimeelezea wasiwasi kwamba, matukio katika eneo la Pembe ya Afrika mpaka Februari mwaka huu (2026) yanaonyesha ongezeko kubwa la mvutano kati ya Misri na Israel.

Mtandao wa Russia El Youm umeinukuu tovuti ya habari ya Kizayuni Natsio Net na kuripoti kwamba matukio katika Pembe ya Afrika hadi Februari 2026 yanaonyesha ongezeko kubwa la mvutano kati ya Misri na utawala wa kizayuni wa Israel kutokana na kuongezeka kwa uingiliaji katika kadhia ya “Somaliland”.

Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti hii ya habari ya Kizayuni hatua ya Israel ya kulitambua rasmi eneo la Somaliland kama nchi huru ilileta mabadiliko makubwa katika matukio ya kikanda, na kuongeza kasi ya kupelekwa vikosi vya kijeshi vya Misri katika Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, inayokadiriwa kuwa takriban askari 10,000, kulionyesha radiamali ya kijeshi ya Cairo kwa hatua ya Tel Aviv.

Kutumwa kwa vikosi vya kijeshi vya Misri kama sehemu ya ujumbe wa Umoja wa Afrika na vingine kama sehemu ya makubaliano ya ulinzi wa pande mbili kumeanza nchini Somalia. Jeshi la Misri pia lilifanya gwaride la kijeshi huko Cairo mnamo Februari 11, 2026, lililohudhuriwa na rais wa Somali na hivyo kutuma ujumbe wa moja kwa moja kwa Israel na Ethiopia.

Ripoti ya Natsio Net inaongeza kuwa Misri imetangaza rasmi kupinga vikali hatua ya Israel ya  kulitambua rasmi eneo la Somaliland kama nchi huru na kuitaja kama tishio kubwa la usalama kwa ufikiaji wa Misri kwenye Bahari Nyekundu na usalama wa taifa wa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *