Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Health Africa Tanzania, Dk Florence Temu afungua kikao cha Nne cha Kamati Tendaji na wadau wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF) 2026 jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana, Rajabu Juma Suleiman, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya DOYODO Tanzania, kikilenga kuimarisha maandalizi kuelekea jukwaa hilo muhimu la kitaifa.

Kikao kimejadili kuimarisha ushirikiano, mipango na mikakati madhubuti ya kuhakikisha jukwaa linawafikia vijana wengi zaidi na kuwafungulia fursa za maendeleo, ubunifu na ushiriki katika ujenzi wa taifa.

Kupitia maandalizi hayo, msingi imara wa jukwaa jumuishi lenye sauti ya vijana na lenye matokeo chanya kwa maendeleo ya vijana nchini unaendelea kuwekwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *